×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Jumwa kusalia rumande hadi Alhamisi atakaposhtakiwa

Jumwa kusalia rumande hadi Alhamisi atakaposhtakiwa

Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa na msaidizi wake Geofrey Otieno watasalia rumande kwa siku nyingine tatu kabla ya kufunguliwa mashtaka ya mauaji Alamisi wiki hii. 

Mahakama ya Mombasa imeagiza wawili hao wasalie rumande ili kupisha muda wa kufanyawi ukaguzi wa akili kabla ya kusomewa mashtaka dhidi yao.

Jaji wa Mahakama ya Mombasa Njoki Mwangi amesema washukiwa hao wanaohusishwa na mauaji ya Ngumbao Jola katika eneo la Ganda kwenye Kaunti ya Kilifi mwaka uliopita watazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Bandari Jijini Mombasa.

Jola aliyekuwa na umri wa miaka 48 aliuliwa wakati wa kampeini ya uchaguzi mdogo wa Ganda mwaka uliopita

Haya yanajiri huku Mahakama ya Machakos ikiratibu Octoba 26 kuwa siku ya kusikiliza vikao vya kesi ya mauaji dhidi ya afisa wa polisi Nancy Njeri ambaye alimkata mkono wakili Onesmus Masaku ambaye alifariki dunia hapo jana. Polisi huyo alikosa kufika mahakamani leo na kuilazamu mahakama kuahirisha vikao.

Wakili Masakau amekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Kenyatta alikokuwa akitibiwa baada ya kukatwa mkono. Mawakili wenzake wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Lower Eastern Justus Mutia wanashinikiza haki kutendeka.