×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

KNEC kuongoza utathmini wanafunzi wa gredi ya 4 na darasa la nane Jumatano

KNEC kuongoza utathmini wanafunzi wa gredi ya 4 na darasa la nane Jumatano

Baraza la Mitiahani Nchini KNEC, litaanza shughuli ya kuwatathmini wanafunzi wa Gredi ya Nnne na Darasa la Nane Jumatano wiki hii.

Baraza hilo limesema mitihani hiyo itafanywa ili kupima uwezo wa wanafunzi ambao wamekuwa nyumbani kwa muda mrefu kutokana na janga la korona.

Mitihani hiyo itafanyika kwa siku tatu kwa watahiniwa wa darasa la nane ambao watafanya masomo yote huku wale wa gredi ya nne wakipimwa uwezo wao kwa masomo ya Hisabati, Kiingereza, Kiswahili, elimu ya mazingira, Sayansi na Teknojojia kwa siku nne.

Watahini wa Darasa la Nane wataanza na somo la Hisabati, Kiingereza na kisha insha ya kiingereza siku kwanza yani Jumatano wiki hii, kisha Sayanzi, Kiswahili na Insha siku ya pili na Somo la Kijamii na dini siku ya mwisho.

Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa KNEC Dakta  Mercy Karogo amesema mitahini hiyo itaandaliwa kuzingatia pahali ambapo selabasi ilikuwa imefikia kabla ya Machi.

Karogo amesema walimu watawafahamisha wanafunzi kwamba haitakuwa mitihani ya kawaida ya kitaifa bali shughuli ya majaribio kutathmini athari za korona katika sekta ya elimu.

Afisa huyo anasema matokeo ya shughuli hiyo yatatumiwa na serikali kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya elimu baada ya kuathirika na makali ya korona.

Wizara ya Elimu iliharisha shughuli hiyo iliyokuwa ianze leo ili kupisha maadhimisho ya Siku ya Mashujaa