×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kaunti ya Nandi yafungwa makao makuu yake kutokana na maambukizi ya korona

Kaunti ya Nandi yafungwa makao makuu yake kutokana na maambukizi ya korona

Makao Makuu ya Serikali ya Kaunti ya Nandi mjini Kapsabet yamefungwa kwa muda wa siku kumi na nne baada ya maafisa wakuu wanane wa serikali ya kaunti hiyo kuambukizwa virusi vya korona.

Kwa mujibu wa Katibu wa Kaunti hiyo Francis Sang wanane hao ni wa Idara za Fedha, Afya vilevile wa Idara ya Elimu. Wafanyakazi katika idara hizo wametakiwa kufanya kazi wakiwa nyumbani huku serikali hiyo ikipanga kuanza kuwapima wafanyakazi wake wanaohudumu mjini Kapsabet.

Maafisa walioathiriwa na korona wametakiwa kujiweka karantini kwa siku kumi na nne kabla ya kufanyiwa vipimo kubaini iwapo wamepona Ugonjwa wa Covid-19, kabla ya kuruhusiwa kurejea ofisini.

Wakati uo huo Sang amewataka wafanyakazi wote wa Kaunti ya Nandi kuhakikisha wanafuata maagizo yaliyowekwa na Wizara ya Afya kudhibiti maambukizi zaidi.

Ikumbukwe Kaunti ya Nandi, Uasin Gishu vilevile Trans Nzoia, Nairobi na Nakuru zimekuwa zikiripoti idadi kubwa ya maambukizi katika siku za hivi karibuni.

Kwenye Kaunti ya Uasin Gishu, Gavana Jackson Mandago ameitisha mkutano wa dharura kujadili kuhusu janga la korona huku akiwataka maafisa wa Idara ya Afya kuhakikisha kila mkazi wa kaunti hiyo anafuata masharti ya kukabili maambukizi.

Share this: