×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Miungano ya wahudumu wa afya wa Nairobi yatoa ilani ya mgomo

Miungano ya wahudumu wa afya wa Nairobi yatoa ilani ya mgomo

Miungano mbalimbali ya wahudumu wa afya jijini Nairobi imetoa makataa ya hadi Octoba 29 kwa Wizara ya Afya na Tume ya Huduma za umma, kushughulikia matakwa yao la sivyo watasitisha huduma kwenye hospitali zote za umma.

Miungano hiyo imelalamikia kupuuzwa kwa mikataba ya makubaliano baina yao na serikali ya kaunti huku wanachama wakiendelea kutaabika hasa wakati huu wa janga la korona.

Miongoni mwa matakwa wanayoshinikiza yatekelezwe ni pamoja na kupandishwa vyeo, kuongezewa mishara na marupurupu na kupewa mazingira mazuri ya kufanyia kazi. Mohamed Duba ni kiongozi wa miungano hiyo

Viongozi wa miungoni hiyo zikiwamo KPMDU za madakatari, ule ya wauguzi KUNU, na CUCO ya maafisa wa kliniki wametaka Wakenya kutotafuta huduma za matibabu katika hospitali za umma ifikiapo Octoba 29.

Haya yanajiri huku Wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Nakuru wamelalamikia mazingira duni ya kufanyia kazi huku wakitishia kusitisha huduma iwapo matakwa yao hayatashughulikiwa kwa haraka.

Wauguzi hao wamesema kwamba Serikali ya Kaunti ya Nakuru imewatelekeza huku wenzao ishirini na wawili wakiambukizwa virusi vya korona kutokana na ukosefu wa vifaa vya kujikinga wanawapowahudumia waathiriwa wa korona.

Wakizungumza leo hii wahudumu hao wamesema kuwa kaunti imekataa kuwapa mafunzo ya kukabili maambukizi ya korona hali inayowaweka katika hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa.

Aidha wanashinikiza shughuli ya kuwafuatilia waliotangamana na waathiriwa kufuatiliwa na kuwekwa karantini.

Vilevile, wameuomba usimamizi wa Hospitali ya Rufaa ya Nakuru kuhakikisha kuwa wagonjwa wanoingia hospitalini humo kutibiwa wanapimwa kubaini iwapo wanavirusi vya korona au la.