×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakili Onesmus Masaku aliyekatwa mikono ameaga dunia

Wakili Onesmus Masaku aliyekatwa mikono ameaga dunia

Wakili Onesmus Masaku wa Kaunti ya Makueni amefariki dunia siku chache tu baada ya kujeruhiwa na afisa wa polisi wa Kituo cha Wote kwa jina Nancy Njeri.

Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria LSK tawi la Lower Eastern Justus Mutia amesema marehemu alifariki dunia akitibiwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.

Hata hivyo, Wakili Mutia amesema LSK itazidi kufuatilia kesi ya Marehemu Wakili Masaku.

Aidha, amerejelea wito wake kwa Wakenya kukoma kujichukulia sheria mikononi wanapokumbwa na matatizo ya kijamii na kuwataka kutafuta usadizi wa viongozi wa dini na wazee.

Awali mshukiwa alidai kwamba alimjeruhi marehemu wakati alipojaribu kumbaka ila madai hayo yakafutiliwa mbali huku ikibainika kwamba tofauti zilitokea baina ya wawili hao kwani walikuwa wapendi.

Ikumbukwe kesi dhidi ya mshukiwa huyo inatarajiwa kutajwa Oktoba 23 baada ya polisi kuomba muda zaidi ya kufanya uchunguzi