×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 685 wameambukziwa korona ;7 wameaga dunia na 105 wamepona

Watu 685 wameambukziwa korona ;7 wameaga dunia na 105 wamepona

Kenya inaelekelekea katika awamu ya pili ya maambukizi ya virusi vya korona. Amesema Waziri wa Afya Mutahi Kagwe.

Akizungumzia kuongezeka kwa watu wanaoambukizwa virusi vya korona tangu kulegezwa kwa masharti ya kudhibiti Korona nchini, Waziri Kagwe amesema viwango vya maambukizi hayo vinazidi kuongezeka kila siku.

Waziri Kagwe amesema idadi ya watu wanaougua COVID-19 wanaolazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi inaendelea kuongezeka vilevile wale wanaolazwa hospitalini.

Leo hii watu mia tisa themanini na watano wamethibitishwa kuambukizwa korona katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Idadi hii imetokana na sampuli elfu nne, mia tisa kumi na mbili zilizopiwa.

Viwango vya maambukizi leo ni asilimia kumi na mbili ikilinganishwa na jana ambapo vilikuwa asilimia 11. 1, na asilimia 4 mapema mwezi huu wakati masharti ya kudhibiti maambukizi yalipolegezwa.

Wakati uo huo, watu wengine mia moja na watano wamepona.

Watu wengine saba wamefariki dunia na kufikisha idadi jumla kuwa mia nane thelathini na wawili.