×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kamati ya Kitaifa inayoshughulikia Korona yafanya mkutano

Kamati ya Kitaifa inayoshughulikia Korona yafanya mkutano

Kuongezeka kwa idadai ya watu wanaoambukizwa virusi vya korona nchini kumeendelea kuibua hofu huku Kamati ya Kitaifa ya Kukabili Janga la Korona ikifanya mkutano leo hii kuhusu suala hilo.

Baadaye alasiri Waziri wa Afya Mutahi Kagwe anatarajiwa kuhutubu kuhusu hali ya korona nchini

Miongoni mwa masuala ambayo Waziri huyo anatarajiwa kuzungumzia ni kuongezeka kwa maambukizi ya korona, hali ya Wakenya kuanza kuyapuuza masharti yaliyowekwa na Wizara ya Afya Kuthibiti virusi hivyo nchini.

 

Katika muda wa takribani wiki tatu sasa kiwango cha maambukizi kimekuwa kikipita asilimia tano huku jana pekee kikiwa asilimia kumi na moja nukta moja hali.

Hayo yanajiri huku, Mamlaka ya Usimamizi wa Jiji NMS ikiendelea kuwapima watu kwa halaiki hapa jijini Nairobi

Watu elfu mbili hamsini na sita walipimwa jana pekee huku idadai hiyo ikitarajiwa kuongezeka leo ikiwa siku ya mwisho.

Takwimu za NMS zinaonesha kwamba Eneo la Makadara ndilo lililorekodi idadi kubw ya watu waliojitokeza kupimwa ambao ni mia mbili arubaini na sana, likifuatwa na Kibra na watu mia mbili na waane, Dagorreti Kusini moa moja tisini na wtatu, Dagoretti Kaskazini mia moja sitini na wanane, Embakasi Kaskazini mia moja thelathini na watano na asarani mia moja ishirini na watano.

Eneo la Roysambu lilirekodi idadi ndogo ambapo ni watu sabini na wawili tu waliopumwa na Ruaraka watu themanini na wawili pekee ndio waliojitokeza.