array(0) { } Radio Maisha | Asilimia 59 ya wanaume wako katika athari yakuwa na shinikizo la damu mwilini
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Asilimia 59 ya wanaume wako katika athari yakuwa na shinikizo la damu mwilini

Asilimia 59 ya wanaume wako katika athari yakuwa na shinikizo la damu mwilini

Mwaka huu maadimisho ya siku ya kuelimisha na kuhamasisha kuhusu shinikizo la damu mwilini yanajiri wakati ambapo janga la COVID-19 limeendelea kuwahatarisha walio na  tatizo hilo.

Janga hili vilevile limeonesha wazi mwanya ulioko katika huduma za afya hasa katika matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza. Hata hivyo, mikakati imewekwa kutatua suala hilo, serikali ikishirikiana na Chama cha Magonjwa yasiyoambukiza NCD Alliance Kenya kuhakikisha wagonjwa wanapokea huduma bora wakati huu wa COVID-19.

Haya yanajiri huku utafiti ukionyesha kuwa asilimia 54.4  wanakaribia kuwa na shinikizo la damu mwilini yaani prehypetension huku asilimia 20.8 wakiwa na shinikizo la damu mwilini. Utafiti huo ambao ulifanyiwa watu milioni 5.9 unaonyesha asilimia 59 ya wanaume wako katika atahri yakuwa na prehyperetension huku wanawake wakiwa asilimia 52. Wote wakiwa miaka 65 na juu. Asilimia 57 wakiwa maeneo ya mashinani huku asilimia 55 wakiwa katika miji.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO preheypetension ni wakati ambapo shinikizo la damu mwili liko kati ya 120/80 na 139/89. Awamu ya  pili ya shinikizo la damu mwlini huwa 140/90, ikifika 180/120 athari ya kupata kiarusi yaani stroke huwa juu zaidi.