array(0) { } Radio Maisha | Kiwango cha asilimia ya maambukizi ya virusi vya korona nchini kimepungua kwa .6%
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kiwango cha asilimia ya maambukizi ya virusi vya korona nchini kimepungua kwa .6%

Kiwango cha asilimia ya maambukizi ya virusi vya korona nchini kimepungua kwa .6%

Na Mate Tongola,

NAIROBI, KENYA, Kiwango cha asilimia ya maambukizi ya virusi vya korona nchini kimepungua kwa asilimia nukta sita na kufikia asilimia 10.1 ikilinganishwa na jana ambapo kiwango hicho kilikuwa asilimia 10.7.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya, idadi ya visa vya maambukizi nchini imeongezeka kwa 437 na hivyo kufikisha idadi jumla ya visa 43,580 tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza nchini.

Idadi hii ni kufatia sampuli 611,552 zilizopimwa chini ya kipindi cha saa 24 zilizopita. Aidha, watu 7 miongoni mwa 437 waliothibitishwa kuambukiwa ni raia wa kigeni huku waliosalia wakiwa Wakenya. 253 ni wanaume huku 184 wakiwa wa jinsia wa kike.

Wagonjwa 140 wameripotiwa kupona na kuruhusiwa kwenye nyumbani, 72 miongoni mwao wakiwa waliokuwa wakitibiwa nyumbani. Kwa sasa, jumla ya waliopona kutokana na ugonjwa wa Covid-19 ni 31,648. Hata hivyo, wagoinjwa wengine 8 wamefariki dunia na hivyo kufikisha 813 idadi jumla ya waliofariki dunia.

Kaunti ya Nairobi ingali inaongoza kwa idadi ya visa vya maambukizi kwa 136 ikifuatiwa na Nakuru 66, Kilifi 29, Kisumu 26, Uasin Gishu 21, Kericho 21, EMbu 17, Busina 16, Kajiado 15, Migori 14, Machakos 14, Kiambu 9 sawa na Meru.