array(0) { } Radio Maisha | Je, ni kweli Jubilee imewafeli Wakenya?
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Je, ni kweli Jubilee imewafeli Wakenya

Je, ni kweli Jubilee imewafeli Wakenya

Na Sam  Amani,

NAIROBI, KENYA, Kauli ya Naibu wa Rais William kuwa ushirikiano baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga umeleza pakubwa utekelezaji wa ahadi zao kwa Wakenya wakati wa kampeni.

Kwa mujibu wa Ruto, Mpango wa Upatanishi BBI ndio ambao umesababisha miradi ya maendeleo kukwama hasa ajenda nne za serikali. Je, matamshi ya Ruto ni ya kweli au ni kwa nini Ruto anailaumu serikali anayoitumikia kwa kushindwa kutekeleza jukumu lake

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Martin Oloo anasema tangu kipindi cha kwanza cha uongozi wa serikali ya Jubilee, imedhihirika wazi kwamba imeshindwa kutekeleza ahadi zake na kwamba siasa za BBI hazijaathiri kwa vyovyote utendakazi wa serikali.

Aidha, Oloo anasema ingekuwa bora zaidi kwa Naibu wa Rais William Ruto kuweka wazi anayemlaumu badala ya kuzielekeza lawama hizo kwa BBI.

Kuhusu hatua ya Kinara wa Chama cha ODM kuhudhuria mkutano wa Baraza la Mawaziri kwenye Kaunti ya Taita Taveta, Oloo anasema upo mkanganyiko katika serikali ya Jubilee, na kwamba kuna udhaifu fulani katika utendakazi wake kiasi cha kumwalika kiongozi wa upinzani.