array(0) { } Radio Maisha | Siku ya Chakula Duniani, je, tuna chakula cha kutosha?
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Siku ya Chakula Duniani, je, tuna chakula cha kutosha

Siku ya Chakula Duniani, je, tuna chakula cha kutosha

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Dunia inapoadhimisha siku ya chakula Ijumaa hii, imebainika kwamba huenda watu zaidi ya milioni mia moja thelathini wakakumbwa na tatizo la uhaba wa chakula ifikiapo mwisho wa mwaka huu.

Shirika la Umoja wa Mataifa limesema kwamba hali hii imechangiwa na kusambaa kwa janga la virusi vya korona, ambalo limeathiri uzalishaji na usambazaji wa chakula katika mataifa mbalimbali.

Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres aidha amesema zaidi ya watu bilioni tatu kote duniani hawana uwezo wa kupata vyakula vilivyo na virutubishi vinavyohitajika kwa afya bora.

Akizungumza kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani inayofanyika Ijumaa Guterres ameyaomba mataifa kuweka mikakati kuhakikisha kwamba wananchi wanapata chakula bora na wanachohitaji.

Humu nchini watu milioni 1.3 wanakabiliwa na uhaba wa chakula huku idadi hiyo ikipungua kutoka watu milioni 2.6 mwaka jana.

Shirika la Msalaba mwekundu linasema ukosefu wa chakula nchini umechangiwa hasa na janga la virusi vya korona, mafuriko na uvamizi wa nzige. Shirika hilo limesema tangu mwezi Machi mwaka huu limetoa msaada wa cahkula kwa zaidi ya familia elfu themanini na tano kote nchini zilizoathirika.