array(0) { } Radio Maisha | TSC yahitaji Ksh4b kuwaajiri walimu 4,000
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

TSC yahitaji Ksh4b kuwaajiri walimu 4,000

TSC yahitaji Ksh4b kuwaajiri walimu 4,000

Na Caren Papai,

NAIROBI, KENYA, Tume ya Huduma za Walimu TSC inahitaji shilingi bilioni nne zaidi kuwaajiri walimu elfu nane kuchukua nafasi ya wale watakaostaafu ifikiapo Desemba mwaka huu.

TSC inasema kwa sasa ina jumla ya shilingi bilioni 2.5 inazolenga kutumia kuwaajiri walimu wengine ikisema hazitoshi na kwamba inahitaji fedha zaidi.

Afisa Mkuu Mtendaji wa TSC Nancy Macharia ameiomba serikali kuharakisha kwani walimu hao watakapostaafu huenda hali hiyo ikaathiri pakuwa matayarisho ya mitihani ya kitaifa inayoratibiwa kuanza Machi mwakani.

Kwa sasa tume hiyo inaendelea kuwaajiri walimu elfu kumi na moja ,mia tano sabini na wanne watakaosadia kufanikisha mpango wa serikali kuhakikisha kwamba asilimia mia moja wa wanafunzi wanaofanya mitihani ya darasa la nane wanajiunga na shule za upili.

Macharia anasema walimu wanaoajiriwa wataripoti shuleni kuanzia Januari mwaka ujao, akisema ni tofauti na elfu nane wanaolengwa.

Aidha ameelezea hofu kwamba huenda shule za humu nchini zikakumbwa na uhaba wa walimu kutokana na janga la korona kwani walio na miaka hamsini na mitano au zaidi hawatahitajika kuripoti shuleni sawa na wenzao hivyo basi kusababisha pengo.

Kulingana na TSC kuna zadi ya walimu elfu hamsini walio na miaka hamsini na mitano na zaidi.