array(0) { } Radio Maisha | Uhuru kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Uhuru kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri

Uhuru kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Rais Uhuru Kenyatta Ijumaa atafanya kikao cha Baraza la Mawaziri kitakachowajumuisha Naibu wake William Ruto na Kinara wa ODM Raila Odinga katika maandalizi ya kuzindua rasmi ripoti ya mwisho ya Mpango wa Upatanishi, BBI.

Jumamosi, viongozi wa mabunge yote mawili na kamati mbalimbali watajumuika na viongozi hao watatu katika kuhakikisha kwamba mapendekezo ya BBI yanapitishwa bungeni.

Maspika Justin Muturi wa Bunge la Kitaifa na mwenzake wa Seneti Ken Lusaka awali walithibitisha kupata mwaliko ambapo pia wenyeviti wa kamati zote ya mabunge na manaibu wao wamealikiwa. 

Inasemakana kwamba Kenyatta na Odinga wanawazia kuhakikisha kuwa ripoti ya BBI inaidhinishwa kupitia bunge badala ya kukusanya saini milioni moja za wananchi na kupata idhini ya mabunge ya kaunti kabla ya kura ya maamuzi .

Aidha, viongozi hao wanalenga kushinikiza katiba kufanyiwa marekebisho kupitia kura ya maamuzi ama bila kura hiyo katika mbinu ya kwanza na mbinu ya pili ikiwa kupitia makundi ya mabunge ili kushikiniza mabadiliko.

Ruto ambaye tayari amesema atapinga mapendekezo ya kuongeza nafasi za kazi amelazimika kuahirisha ziara yake kwenye Kaunti ya Murang'a Jumamosi ili ahudhuria kikao hicho.

Akizungumza katika Kaunti ya Nyamira, Ruto aliyakosoa mapendekezo ya BBI hasa kuhusu kuongezwa kwa nafasi zaidi za uongozi huku akisema kwamba hayawezi kumsaidia Mkenya wa kawaida.

Wandani wake wakiongozwa na Seneta wa Elgeyo Marakwet, Kipchumba Murkomen wamekosoa namna vikao vya leo na kesho vitafanyika wakisema ni watu wachache tu wamehusishwa.