array(0) { } Radio Maisha | Idadi ya walifariki dunia kutokana na Korona yapita watu 800
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Idadi ya walifariki dunia kutokana na Korona yapita watu 800

Idadi ya walifariki dunia kutokana na Korona yapita watu 800

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, Kiwango cha asilimia ya maambukizi ya virusi vya korona nchini kimeendelea kuongezeka licha ya shughuli za kawaida kuonekana kurejelewa nchini zikiwemo shughuli za masomo.

Kiwango hicho kimeongezeka kwa asilimia nukta tatu na kufikia asilimia 10.7 ikilinganishwa na asilimia 10.4 Jumatano.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya, watu wengine 602 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Korona chini ya kipindi cha saa 24 zilizopita. Idadi hii imetokana na sampuli 5,618 zilizopimwa na hivyo kufikisha 43,143 idadi ya wanaougua ugonjwa wa Covid-19 nchini.

Aidha, wagonjwa wengine 80 wameripotiwa kupona na hivyo kufikisha 31,508, idadi ya waliopona tangu janga hilo kuripotiwa nchini mapema mwezi Machi mwaka huu. 56 miongoni mwao walikuwa wakitibiwa mwakwo.

Kwa mujibu wa takwimu za leo, kaunti ya Nairobi inaongoza kwa idadi ya maambukizi ikiwa ni visa 133 huku mwathiriwa mchanga zaidi akiwa mtoto wa mwaka mmoja huku mkongwe zaidi akiwa wa umri wa miaka 93.

Hata hivyo, watu wengine wanane wameripotiwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.