array(0) { } Radio Maisha | Ruto aendeleza shutma dhidi ya Matiang'i
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ruto aendeleza shutma dhidi ya Matiang'i

Ruto aendeleza shutma dhidi ya Matiang'i

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Naibu wa Rais William Ruto ameendeleza shtuma dhidi ya Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Fred Matiang'i akisema alikuwa na njama ya kumzuia kufanya ziara kwenye maeneo ya Kisii hasa baada ya mkutano wake kutibuliwa kwenye Kaunti ya Nyamira juma lililopita.

Akihutubu kwenye eneo la Sironga wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kwa makundi ya wanabodaboda kwenye eneo hilo, Ruto amesisitiza kwamba ataendelea kuwasaidia Wakenya wenye kipato cha chini.

Ruto ambaye ameyakosoa mapendekezo kwenye mpango wa Upatanishi BBI hasa kuhusu kuongezwa kwa nafasi zaidi za uongozi, amesema hayawezi kumsaidia Mkenya wa kawaida.

Wakati uo huo, ameendeela kuwashauri vijana kutokubali kutumika na wanasiasa kuzua fujo.