array(0) { } Radio Maisha | Karua aikosoa serikali kwa kutatiza baadhi ya mikutano ya hadhara
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Karua aikosoa serikali kwa kutatiza baadhi ya mikutano ya hadhara

Karua aikosoa serikali kwa kutatiza baadhi ya mikutano ya hadhara

Na Mate Tongola,

NAIROBI, KENYA, Wizara ya Masuala ya Ndani ya Nchi imeendelea kushutumiwa kufuatia hatua ya kubagua mikutano ipi ya kisiasa inapaswa kuendeshwa nchini.

Kiongozi wa Chama cha Narc Kenya Martha Karua amesema kwamba hatua ya Baraza la Kitaifa la Ushauri kuhusu Masuala ya Usalama ya kuweka masharti ya kutimizwa kabla ya kuandaliwa kwa halfa za hadhara na ukiukaji mkubwa wa sheria na uhuru wa kuzuru maeneo yoyote nchini, kwa mujibu wa Katiba.

Akihutubu katika Makao Makuu ya chama hicho hapa Nairobi, Karua aidha amesema kwamba polisi wanajukumu la kuwapa ulinzi raia wote bila ubaguzi.

Kauli yake inajiri wiki moja tu baada ya ziara ya Naibu wa Rais William Ruto kwenye Kaunti ya Nyamira kusitishwa kabla ya kuruhusiwa.