×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

KNEC yapinga mpango wa kuwahamisha watahiniwa 1.9m

KNEC yapinga mpango wa kuwahamisha watahiniwa 1.9m

Na Caren Papai,

NAIROBI, KENYA, Baraza la Mitihani Nchini, KNEC limepinga mpango wa kuwahamisha watahiniwa milioni 1.9 wa Darasa la nane na kidato cha nne.

Haya yanajiri baada ya baadhi ya wazazi kusema watawahamisha wanao kutoka shule za mabweni  au zile za binafsi kwa kushindwa kuwalipia karo. Aidha, wazazi wengine wamewahamisha wanao kutoka shule zenye idadi kubwa ya wanafunzi ili kusadia kuthibiti maambukizi ya virusi vya korona.

Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi Nicholas Maiyo amesema hatua hiyo imechangiwa na ugumu wa maisha ambao umetokana na janga la korona.

Kauli hii imejiri wakati ambapo serikali imesema itawahamisha zaidi ya wanafunzi elfu saba kutoka jumla ya shule kumi na saba ambazo zimeathirika na mafuriko katika kaunti ya Baringo.

Kulingana na KNEC usajili wa watahiniwa umekamilika, hivyo basi watahitajika kufanyia mitihani katika vituo ambavyo walisajiliwa ili kuepuka mkanganyiko ambao huenda ukatokea baadaye.

Ratiba ya KNEC inaonesha kwamba mitihani ya KCPE itaanza tarehe 22 Machi na kukamilika tarehe 24, siku moja kabla ya ile ya KCSE kuanza. Shughuli ya usahihishaji itafanyika kati ya tarehe 19 Aprili na Mei tarehe 7.

Kuna watahiniwa milioni 1.2 wa KCPE na elfu mia saba hamsini na moja, mia moja hamsini wa KCSE waliosajiliwa.