array(0) { } Radio Maisha | Jopo la majaji kuamua hatma ya Bunge
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Jopo la majaji kuamua hatma ya Bunge

Jopo la majaji kuamua hatma ya Bunge

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Hatma ya wabunge sasa i mikononi mwa jopo la majaji watano lililobuniwa kusikiliza kesi zinazopinga ushauri wa Jaji Mkuu David Maraga kwamba bunge livunjwe kwa kushindwa kupitisha mswada wa thuluthi mbili wa uwakilishi sawa wa kijinsia.

Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu amebuni jopo hilo likaloongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Lydia Achode huku wanachama wengine wakiwa George Odunga, James Makau, Pauline Nyamweya na Anthony Ndung'u.

Jopo hilo limebuniwa kufuatia uamuzi uliotolewa na Jaji wa mahakama Kuu  Weldon Korir.

Mahakama ilisitisha kutekelezwa kwa ushauri huo kufuatia kesi ya Wakenya wawili Lenna Konchela na Abdul Munasa waliuopinga wakisema kwamba sheria ilipuuzwa.

Majaji hao watano wanalenga kusikiliza kesi zaidi ya tano kuhusu suala hilo, ambazo ni kesi iliyowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Paul Kihara Kariuki, Tume ya Huduma za Bunge, Seneti, Mbunge wa Mathare Antony Oluoch na wakili Adrian Kamotho ambao wanapinga kuvunjwa kwa bunge

Hayo yanajiri huku baadhi ya mashirika na makundi mbalimbali kikiwamo Chama cha Wanasheria LSK, kikiunga mkono pendekezo la Maraga, huku Kihara akiwa na mtazamo tofauti akisema Maraga amepuuza haki za Wakenya na kwamba sheria haijaweka wazi kuhusu hatua ya kuvunjwa  kwa bunge.