×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu wengine 604 waambukizwa korona nchini Kenya

Watu wengine 604 waambukizwa korona nchini Kenya

Baada ya asilimia 12.3 ya kiwango cha maambukizi ya korona kutangazwa jana, leo hii kiwango hicho ni asilimia 10.4. Watu wengine 604 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona baada ya kupimwa kwa sampuli elfu tano, mia nane na mbili katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Idadi jumla ya walioambukizwa nchini sasa imefikia elfu arobaini na mbili, mia tano arobaini na mmoja. Miongoni mwa walioambukizwa, mia tano themanini na watatu ni Wakenya huku raia wa kigeni wakiwa 21. Mia nne miongoni mwao ni wanaume na wanawake 204. Mtu mchanga zaidi aliyeambukizwa ni mtoto wa umri wa miezi mitano huku mzee zaidi akiwa na miaka tisini na minne.

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa maambukizi mia moja ishirini na matano, Nakuru 113, Mombasa 87, Busia 35, Uasin Gishu 33, Trans Nzoia 25 sawa na Kiambu, kwenye Kaunti ya Kisii watu 24 wameambukizwa, Kisumu 24, Kajiado 16, Nandi 13, Kakamega 12, Meru 11, Machakos 7, Siaya 7 sawa na Garissa huku kaunti za Murang'a Pokot Magharibi na Nyeri zikiwa na watu watano walioambukizwa katika kila kaunti.

Turkana walioambukizwa ni 4, Laikipia 3 sawa na Wajir, Embu 2, Kirinyaga 2 Narok 2 sawa na Taita Taveta. Kaunti za Kitui, Nyamira, Tharaka, Kilifi na Nyandarua zina kisa kimoja kimoja.

Watu wengine 88 wamepona virusi vya korona ambapo 56 miongoni mwao ni waliokuwa wakihudumiwa myumbani huku 32 wakiwa wale waliokuwa hospitalini, hali inayofikisha elfu 31, 428 idadi jumwa ya waliopona kuwa. Hata hivyo watu wengine 10 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid 19 na kufikisha 797 idadi ya waliofariki dunia.