×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mikakati dhabiti yapendekezwa kukabili magonjwa yasiyoambukiza

Mikakati dhabiti yapendekezwa kukabili magonjwa yasiyoambukiza

Utafiti uliofanywa na Shirika la Kitaifa la Takwimu KNBS, umebainisha kwamba wakati huu wa janga la COVID-19 asilimia 17 ya familia zilikuwa na angalau mtu anayeugua magonjwa yasiyoambukiza, Shinikizo la damu likiongoza kwa asilimia 34, kisukari asilimia 19.9, pumu asilimia 16.7, magonjwa mengine yasiyoambukiza asilimia 14.5, saratani asilimia 2.

Kuhusu magonjwa yanayoambukiza, utafiti huo ulibainisha kuwa asilimia 5.2 wana virusi vya HIV, asilimia 4.5 matatizo ya mapafu, na kifua kikuu asilimia 3.4.

Katika kikao cha mtandao na wanahabari, Mshauri katika Chama cha Kitaifa cha Magonjwa yasiyo ya kuambukiza NCD Alliance of Kenya NCDAK, Catherine Karekezi, amesema kuwa serikali inastahili kuweka mikakati ya kushughulikia walio na magonjwa yasiyoambukiza kwani magonjwa hayo husababisha asilimia 55 ya vifo na asilimia 50 ya wanaolazwa hospitalini.

Katika kikao hicho, daktari Eva Njenga ambaye ni Mwenyekiti wa NCDAK amesema kuwa Bima ya Kitaifa ya Afya, NHIF imeweka mikaktai ya kuhakikisha wanaotafuta huduma za afya wanapunguziwa mzigo na ada inayolipwa.