×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Jopo lakusikiliza ushauri wa Maraga kuhusu kuvunjwa kwa bunge labuniwa

Jopo lakusikiliza ushauri wa Maraga kuhusu kuvunjwa kwa bunge labuniwa

Jopo la majaji wa watano li tayari kuanza kusikiliza kesi kuhusu ushauri wa Jaji Mkuu David Maraga kwa Rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge kwa kushindwa kupitisha Mswada wa Thuluthi Mbili ya Uwakilishi wa Kijinsia.

Jipo hilo limeteuliwa na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu na litaongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu Lydia Achode huku wanachama wengine wakiwa George Odunga, James Makau, Pauline Nyamweya na Anthony Ndung'u.

Hatua hii imejiri baada ya Jaji Weldon Korir kuagiza kubuniwa kwa jopo hilo kufuatia ushauri wa Maraga kutaka bunge livunjwe kwa kutelekeza majukumu yake.

Mahakama ilisitisha kutekelezwa kwa ushauri huo wa Maraga kufuatia kesi ya Wakenya wawili Lenna Konchela na Abdul Munasa waliuopinga wakisema kwamba sheria ilipuuzwa. Majaji hao watano wanalenga kusikiliza kesi zaidi ya tano kuhusu suala hilo.

Miongoni mwayo ni kesi iliyowasilishwa na Mkuu wa Sheria Kihara Kariuki, Tume ya Huduma za Bunge, Seneti, Mbunge wa Mathare Antony Oluoch na wakili Adrian Kamotho ambao wanapinga kuvunjwa kwa bunge

Baadhi ya mashirika na makundi mbalimbali kikiwamo Chama cha Wanasheria LSK, kimeunga mkono pendekezo la Maraga.