×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mbunge Aisha Jumwa kufunguliwa mashtaka ya mauaji

Mbunge Aisha Jumwa kufunguliwa mashtaka ya mauaji

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Noordin Haji ameidhinisha Mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Jumwa na mlinzi wake Godfrey Okuto wanatuhumiwa kumuua mmoja wa wafuasi wa ODM katika Wadi ya Ganda, Kilifi mwaka uliopita.

Haji anasema ofisi yake imeshirikiana na Ofisi ya Mshikirishi wa Uslalama katika Kaunti ya Mombasa, Alloys Kemo kufanya uchunguzi dhidi ya Jumwa na Okuto.

Kwa mujibu wa Haji, upo ushahidi wa kutosha kuwashtaki wawili hao.

Jumwa anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiakili juma lijalo kabla ya kuwasilishwa mahakamani. Wawili hao walifikishwa mahakamani mwaka uliopita, na kuachiliwa kwa dhamana bila kushtakiwa.