array(0) { } Radio Maisha | Jeshi la KDF lapongezwa katika juhudi za kukabili Al Shabaab
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Jeshi la KDF lapongezwa katika juhudi za kukabili Al Shabaab

Jeshi la KDF lapongezwa katika juhudi za kukabili Al Shabaab

Waziri wa Ulinzi, Monica Juma amepongeza juhudi za utendakazi wa Jeshi la Ulinzi KDF za kuendelea kutoa ulinzi kwa taifa dhidi ya mashambulio ya Al - Shabaab.

Akihutubu wakati wa madhimisho ya tisa ya kila mwaka ya Siku ya KDF katika kambi ya Mariakani Garrison kwenye Kaunti ya kilifi, Juma amesema kwamba kulinganishwa na awali jeshi hilo limefanikiwa kuwakabili magaidi kabla ya kutekeleza uvamizi.

Juma vilevile amelipongeza jeshi hilo kwa kuwa mstari wa mbele katika kukabili majanga mbalimbali ambayo yamekuwa yakilikumba taifa yakiwamo mafuriko na maporomoko ya ardhi.

Amesema Wizara yake itaendelea kuhakikisha usalama zaidi unaimarishwa kwenye mipaka ya Kenya na mataifa jirani ili kuzuia biashara haramu.

Awali, Waziri alizindua mnara wa kumbukumbu ya majeshi waliofariki wakiwa kazini, uzinduzi ambao umefanyika katika kambi hiyo. Kaulimbiu ya madhimisho ya mwaka huu ni Kuimarisha Amani na Usalama kupitia Ushirikiano wa Kijeshi na Raia.

Ikumbukwe maadhimisho ya kwanza yalifanyika mwaka wa 2012 kufuatia uzinduzi wa Oparesheni Linda Nchi uliofanyaki Oktoba 12  mwaka wa 2011.