×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Seneti yaelezwa kwamba janga la korona liliathiri maamuzi mbalimbali kwenye kauntii

Seneti yaelezwa kwamba janga la korona liliathiri maamuzi mbalimbali kwenye kauntii

Shughuli katika mabunge ya kaunti ziliathirika kufuatia maambulizi ya virusi vya korona nchini. Muungano wa mabunge ya kaunti umeiambia seneti kwamba, kufuatia kupigwa marufuku kwa mikutano ya umma, baadhi ya maamuzi yalifanywa bila kuwahusisha wananchi inavyohitajika.

Mwenyekiti wa muungano huo, Ndegwa Wahome amesema baadhi ya wafanyakazi wa serikali za kaunti pia walizembea kwa kuwa walifahamu kwamba hawawezi kutakiwa kufika mbele ya kamati za bunge hizo kujieleza.

Wakati uo huo, amesema kwamba kuna baadhi ya maamuzi yaliyofanywa na magavana kama vile kuhusu matumizi ya fedha bila kuyahusisha mambunge hayo.

Wahome sasa anaitaka Seneti kuzichunguza serikali za kaunti kubaini pesa zilizotolewa kwa matumizi kuhusu maambukizi ya korona zilivyotumika.

Ameyasema hayao alipowasilisha ripoti mbele ya kamati ya seneti inayoshughulikia maambukizi ya korona nchini kuhusu jinsi kaunti zinavyoshughulikia tatizo hilo.