×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wandani wa Ruto wataka ICC kumchunguza Mutyambai

Wandani wa Ruto wataka ICC kumchunguza Mutyambai

Wandani wa Naibu wa Rais, William Ruto sasa wanataka Inspekta Mkuu wa Polisi, Hillary Mutyambai kuchunguzwa katika Mahakama ya Jinai, ICC kufuatia mauaji ya watu wawili kwenye Kaunti ya Murang'a wakati wa ziara ya Ruto.

Wametaja mauaji ya wawili hao kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na jamii ya kimataifa inapaswa kuingilia kati ili kukomesha visa vya mauaji nchini.

Viongozi hao aidha wanasema maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Kitaifa ya Usalama kuhusu mikutano ya kisiasa yanalenga kuwakandamiza wandani wa Ruto, na ni kinyume na sheria.

Wakizungumza katika hafla ya mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ukuzaji wa Majani Chai, KTDA Wilfred Murigu, kwenye eneo la Kiamusheru Kaunti ya Nyeri, viongozi hao wamesema hawatakubali kukandamizwa na polisi. Kimani Ichung'wa ni Mbunge wa Kikuyu.

Kauli yake imetiliwa mkazo na Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro ambaye ameendelea kuwasuta wandani wa Rais Uhuru Kenyatta kwa kuwatumia vijana kuvuruga mikutano ya Naibu wa Rais. Aidha, Nyoro kwa mara nyingine amewasuta Mutyambai, Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Dakta Fred Matiang'i na Katibu wake Karanja Kibicho kwa kuwatumia polisi kuwahangaisha wandani wa Ruto.

Kauli yao inajiri wakati ambapo Mutyambai amekana madai hayo akisema kufutiliwa mbali kwa mikutano ya Ruto ni kwa sababu inatishia usalama. Kwa mujibu wa Mutyambai, mikutano ya mahasimu wake haitishii usalama wa Wakenya hivyo basi kuruhusiwa kuendelea.