×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kalonzo awataka Ruto na Raila kujitayarisha kwa kivumbi kikali Msambweni

Kalonzo awataka Ruto na Raila kujitayarisha kwa kivumbi kikali Msambweni

Kinara wa Chama cha Wiper,  Kalonzo Musyoka amehimiza kuondolewa kwa dhana kwamba kinyang'anyiro cha kiti cha ubunge cha Msambweni ni cha kudhihirisha ubabe baina ya Naibu wa Rais, William Ruto na Kinara wa ODM, Raila Odinga. Akizungumza baada ya Chama cha Wiper kumwidhinisha Mohamud Abdulrakman kuwania kiti hicho, Kalonzo amewataka Ruto na Raila kujitayarisha kwa kivumbi kikali akielezea imani kwamba Mohamud ataibuka na ushindi.

Mbali na hayo, Kalonzo amewahimiza maafisa wa polisi kutotumiwa kusuluhisha tofauti za kisiasa miongoni mwa viongozi na kuwataka kutekeleza jukumu lao kwa uadilifu. Amesema usawa unastahili kudumishwa kwa viongozi wote wanapotafuta idhini ya kufanya mikutano yao huku akiwahimiza wanasiasa kuzingatia masharti waliyopewa.