×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Karua amtaka Rais Kenyatta kumheshimu Naibu wake William Ruto

Karua amtaka Rais Kenyatta kumheshimu Naibu wake William Ruto

Kinara wa Chama cha NARK Kenya, Martha Karua amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kushirikiana na Naibu wake William Ruto la sivyo ajiuzulu ili uchaguzi mwingine kufanywa kumchagua Rais mpya.

Kwa mujibu wa Karua, hatua ya Rais Kenyatta kutomheshimu naibu wake ni ishara tosha kwamba haheshimu ofisi ya Rais hasa ikizingatiwa walichaguliwa pamoja.

Karua anasema ofisi ya Rais inajumuisha Rais na Naibu wake, hivyo wawili hao wanastahili kufanya kazi kwa pamoja au wajiuzulu mara moja.

Karua anasema Rais anaonesha mfano mbaya kwani wandani wake wamekuwa wakimrushia naibu wake cheche za matusi kutokana na kimya chake.

Wakati uo huo, Karua amefutilia mbali mashinikizo ya wandani wa Rais Kenyatta kutaka Naibu wa Rais ajiuzulu kwa madai ya kumkosea heshima Rais na kushindwa kuwahudumia wananchi huku akiendeleza siasa za mwaka wa 2022. Karua amemlaumu Rais Kenyatta kwa kumtelekeza naibu wake ilhali katiba inawahitaji wafanye kazi pamoja.

Pia ametaja kuwa kinaya msamaha wa Rais Kenyatta siku ya Jumamosi wakati wa Maombi ya Kitaifa katika Ikulu, akisema yalilenga kumdhalilisha naibu wake.

Karua vilevile ametilia shaka uongozi wa Kenyatta akisema anatoa mfano mbaya kwa mawaziri na magavana ambao tayari wameanza kuwadhalilisha manaibu wao, jinsi anavyomdhalilisha Ruto.