×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Afueni kwa Eve Malenya baada ya kurejeshewa wadhifa wa Uwakilishi Wadi Maalumu Nairobi

Afueni kwa Eve Malenya baada ya kurejeshewa wadhifa wa Uwakilishi Wadi Maalumu Nairobi

Baada ya kuwa nje ya uongozi kwa kipindi cha mwaka mmoja, Mwakilishi Wadi Maalum kwenye Kaunti ya Nairobi wa Chama cha ODM, Eve Malenya ameejeshewa wadhifa huo.

Malenya amerejea wadhifa huo kufuatia agizo la mahakama baada ya kutimuliwa mwezi Aprili mwaka uliopita ambapo alitemwa na Bunge la Kaunti ya Nairobi na hivyo kunyimwa mshahara na marupurupu mengine yanayotengewa wawakilishi wadi.

Spika wa Bunge hilo, Benson Mutura amethibitisha kurejea kwa Malenya katika bunge hilo baada ya Mahakama kusitisha agizo lilichopishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali tarehe 5 mwezi Aprili likiagiza wadhifa wake kutwaaliwa na Perpetua Mponjiwa.

Masaibu yake yalianza mapema mwaka 2017 baada ya jina lake kuondolewa katika sajili ya Wawakilishi Wadi Maalum ya Tume ya Uchaguzi, IEBC.