×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais na naibu wake watakiwa kuwashauri wandani wao ili kutuliza joto la kisiasa

Rais na naibu wake watakiwa kuwashauri wandani wao ili kutuliza joto la kisiasa

Askofu wa Dayosisi ya Kitale, Anthony Crawley amemrai Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake  William Ruto kutuliza joto la kisiasa linaloendelea kupanda kila kuchao kwa kushirikiana kikamilifu na kuwashauri wandani wao kusitisha cheche za maneno yanayoweza kutatiza utangamano uliopo.

Wakati wa kikao na wanahabari ofisini mwake, Crawley amesema Rais ni ishara ya umoja wa taifa na hivyo moyo wa kusamehe jinsi alivyofanya Kenyatta ni wa kuigwa na viongozi na Wakenya wa kawaida.

Kadhalika ameihimiza serikali tendaji na idara ya mahakama kuusitisha mvutano wa mara kwa mara ili kutoa mfano mwema kwa mataifa ya Afrika Mashariki na na bara zima la Afrika.