×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Asilimia 70 ya wakazi Nairobi wanahofia kuwarejesha wanao shuleni-TIFA

Asilimia 76 ya wakazi wa Nairobi wana watoto wanaoenda shuleni kulingana na ripoti ya Shirika la Utafiti la TIFA.

Aidha, asilimia 40 ya wanafunzi walinufaika na masomo yaliotolewa kupitia mitandao ya kijamii, runinga, redio na hata wale waliotumia simu. Asilimia 36 walipata kupitia runinga, asilimia 34 simu na asilimia 11 kupitia vituo vya redio.

Ripoti hiyo imebainisha kwamba asilimia 70 ya wakazi wa Nairobi wenye kipato cha chini wanahofia kuwaruhusu wanao kurejea shuleni, wakiogopa huenda wakaambukizwa virusi vya korona.

Walio na hofu hata zaidi ni wanawake kwa asilimia 73, wanaume wakiwa kwa asilimia 67. Vilevile asilimia 44 ya wazazi wanahofia huenda wakaambukizwa virusi hivyo na wanao wanaporejea nyumbani kutoka shuleni. Kiwango cha hofu ni ya juu zaidi miongoni mwa wanawake kwa asilimia 51, wanaume 35.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo aidha, dhulma ziliripotiwa msimu huu wa korona ambapo asilimia 37 ya wanawake walidhulumiwa na waume zao, huku asilimia 29 wakiripoti kupigwa na wake zao.

Asilimia 25 ya wanawake waliripoti kupigwa, asilimia 20 kupokea cheche za matusi, asilimia 52 wakipokea dhulma zote hizo. Miongoni mwa wanaume, asilimia 26 walipigwa, 30 wakatusiwa, na 39 kupigwa na kutusiwa kwa pamoja.

Aidha, asilimia 22 ya visa vya ulawiti, ubakaji, unajisi miongoni mwa dhuluma nyingine viliripotiwa miongoni mwa watoto wadogo.

Asilimia 28 ya watoto waliripoti kupigwa na wazazi, familia na hata majirani. Asilimia nyingine 21 waliripoti kupokea cheche za matusi kutoka kwa watu wanaowajua, huku asilimia 46 wakiripoti kupokea cheche za matusi vilevile kupigwa.

Ripoti hii kulingana na TIFA ilitolewa kwa mara ya kwanza tarehe 7 Julai Rais Uhuru Kenyatta alipotangaza kwamba shule za msingi na upili zitasalia kufungwa hadi mwezi Januari mwaka ujao.

Aidha, ripoti ya leo ilitolewa tarehe 6 mwezi huu, Waziri wa Elimu Profesa George Magoha alipotangaza kwamba wanafunzi wa gredi ya nne, darasa la nane na wale wa kidato cha nne wanapaswa kurejea shuleni kuanzia jana.