×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Awamu ya pili ya maambukizi ya korona kushuhudiwa katika kaunti za Nairobi na Mombasa

Awamu ya pili ya maambukizi ya korona kushuhudiwa katika kaunti za Nairobi na Mombasa

Huenda kukashuhudiwa awamu ya pili ya maambukizi ya virusi vya korona katika kaunti za Nairobi na Mombasa kufuatia idadi ya juu ya maambukizi katika siku za hivi karibuni.

Aga Khan Hospital imebainisha kwamba idadi ya juu ya mamabukizi ya ndani kwa ndani yameripotiwa jijini Nairobi na viunga vyake, hali inayoashiria  awamu ya pili ya maambukizi. Kwa mujibu wa hospitali hiyo, idadi ya juu ya maambukizi inatokana na mapuuza ya Wakenya ambao wameacha kuvaa maski katika maeneo ya umma.

Afisa Mkuu Mtendaji wa hospitali hiyo Dakta Majid Twahir anasema kwa sasa kaunti za Nairobi na Mombasa zinaripoti visa vya juu kulinganisha na kaunti nyingine nchini, hali inayohatarisha maisha ya wakazi.

Wakati uo huo, Daktari Andrew Were wa Muungano wa Madaktari nchini amepuuza kauli ya serikali kwamba taifa halijaanza kuripoti awamu ya pili ya maambukizi.

Amesema Kaunti ya Bungoma vilevile inaripoti awamu ya pili hasa eneo la Kanduyi ambapo visa hivyo vimeongezeka katika siku chache zilizopita. Katika kipindi cha siku saba zilizopita. watu elfu mbili, mia moja kumi na tisa wameambukizwa virusi vya korona, kulinganishwa na wiki saba za mwezi uliopita ambapo watu elfu moja, mia tatu kumi na watatu waliambukizwa.

Kati ya Oktoba 5 na Oktoba tarehe 11, taifa liliandikisha asilimia 7.4 ya maambukizi kote nchini. Jumapili wiki hii, asilimia 9 ya maambukizi iliripotiwa baada ya watu mia tatu themanini na wanane kuambukizwa korona kutokana na sampuli elfu nne, mia mbili themanini na saba.

Jana taifa lilipoti vifo kumi na kimoja na kufikisha jumla ya waliofariki kufuatia makali ya Covid-19 kuwa 777. Watu wengine sabini na watatu wakiambukizwa korona na kufikisha jumla ya maambukizi kuwa 41, 619.