×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Trump arejelea kampeni tangu kugunduliwa kuwa na korona

Rais Trump arejelea kampeni tangu kugunduliwa kuwa na korona

Kampeni za urais nchini Marekani zimeendelea kushika kasi huku Rais wa taifa hilo Donald Trump akirejea tena kwenye kampeni na kuhudhuria mkutano wa kwanza katika jimbo la Florida siku kadhaa tangu alipogundulika na maambukizi ya virusi vya corona.

Trump aliwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la wazi mjini Sanford; Florida bila ya kuvaa barakoa.

Inaarifiwa kwamba jimbo la Frlorida ni muhimu kwa Trump kushinda na mkutano huo ni moja wapo ya nyingine iliyoratibiwa kufanyika wiki hii kwenye majimbo ya Pennsylvania, Lowa na North Carolina.

Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake waliosimama bega kwa bega wengi wakiwa bila barakoa, Trump amesema afya yake imeimarika na yuko huru kukutana tena na wapiga kura bila ya kuwa na wasiwasi wowote