×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwanamme aliyemteketeza mkewe atiwa mbaroni huko Bomet

Mwanamme aliyemteketeza mkewe atiwa mbaroni huko Bomet

Polisi wamemtia mbaroni Robert Tonui, mwanamme aliyemuua mkewe kwa kumteketeza wiki moja iliyopita kwenye Kaunti ya Bomet.

Kulingana na Kamanda wa Polisi Alex Shikondi, Tonui amekamatwa katika Kaunti ya Kericho, akiwa mafichoni na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho ili kufunguliwa mashtaka.

Wiki iliyopita, Tonui mwenye umri wa miaka hamsini, seremala katika Soko la Seanin, Bomet alimteketeza mkewe Emmy Chepkoech Mitey.

Mkewe ambaye ni Naibu Mwalimu mkuu katika shule moja kwenye Kaunti ya Bomet, alikuwa ameondoka nyumbani kwake kufuatia mzozo na mumewe ila akarejea wiki tatu baadaye ambapo mumewe alimteketeza kwa kutumia mafuta ya petroli.

Majirani walimkimbiza katika Hospitali ya Kimishonari ya Litein ila akafariki akipokea matibabu.