×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

DPP apinga tetesi za kuficha ushahidi unaomhusisha na ufisadi Gavana Ojaamong

Mkuu wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji amepinga tetesi kwamba ameficha ushahidi dhidi ya Gavana wa Busia Sospeter Ojaamong katika kesi ya ufisadi ya shilingi milioni 8.

mmoja wa waendesha mashtaka katika ofisi ya Haji, Grace Murungi amesema Ojaamong na maafisa wengine wanane wana kesi ya kujibu kwa mujibu wa ushahidi waliokusanya kufikia sasa.

Awali, gavana huyo alidai kwamba Haji alikuwa akiipotosha mahakama kwa kuficha baadhi ya stakabadhi anazodai zina ushahidi dhidi yake. Aidha, anaulaumu upande wa mashtaka kwa kutoweka wazi baadhi ya stakabadhi hizo a hivyo kulemaza mpango wa upande wa utetezi kumtetea.

Miongoni mwa stakabadhi hizo ni mpango wa ununuzi wa mali ya umma kwenye serikali ya Kaunti ya Busia, suala ambapo Haji amepinga vikali.