×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Iwapo nimekukosea naomba msamaha -Rais Uhuru Kenyatta

Iwapo nimekukosea naomba msamaha -Rais Uhuru Kenyatta

''Iwapo kuna  mtu ambaye nimemkosea basi ninaomba msamaha'' ndiyo Kauli ya Rais Uhuru Kenyatta alipoongoza hafla ya Moambi ya Kitaifa katika Ikulu ya Nairobi. Rais aidha amesema amewasamehe wote waliomkosea akisema kilicho muhimu kwa taifa hili ni amani hasa miongoni mwa viongozi.

Wakati uo huo, Rais amewashukuru Wakenya wa matabaka mbalimbali wakiwamo viongozi wa makanisa wahudumu wa afya ambao wamekuwa katika mstari wa mbele kuwahudumia Wakenya wakati huu wa janga la virusi vya korona huku akisema kwamba ushirikiano baina ya viongozi nchini bila kuzingatia tiofauti za kisiasa umechangia pakubwa kuendelea kudumisha amani.

Kauli ya Rais leo inajiri wakati ambapo kumeshughudiwa migawanyiko mikali ndani ya chama chake cha Jubilee baina ya wafuasi wanaomuunga mkono na wale wanaomuunga Naibu wake William Ruto.

Hafla hii imefanyika sambamba na maahimisho ya siku ya Huduma ambayo ilitangazwa na serikali kuwa ya Mapumziko ya kitiafa.

Maombi ya leo yamekuwa ya kuliombea taifa hili kwa ajili ya umoja, Mgawanyiko wa Kisiasa, Ufisadi na Matamanio. Viongozi wa madhehebu mbalimbali wameiongoza hafala yenyewe ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa akiwamo Naibu wa rais William Ruto vile vile mawaziri.