×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Huduma za maji kuathirika kwenye maeneo ya Barabara Kuu ya Mombasa

Huduma za maji kuathirika kwenye maeneo ya Barabara Kuu ya Mombasa

Huduma za maji zinatarajiwa kuathirika kwenye maeneo mbalimbali yanayopakana na Barabara Kuu ya Mombasa kuanzia kesho saa kumi na mbili asubuhi hadi Jumapili saa kumi na mbili asubuhi ili kutoa nafasi ya ujenzi wa barabara ya moja kwa moja kutoka Uwanja wa Kitaifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta, JKIA hadi Westlands jijini Nairobi.

Meneja Mkurugenzi wa Kampuni ya Maji ya Nairobi, Nahashon Muguna amesema mabomba ya kusafirisha maji hayo yatafungwa kisha kuunganishwa na mengine mapya.

Miongoni mwa maeneo ambayo huduma za maji zitakatizwa ni Uwanja wa JKIA, Reli ya Kisasa, SGR, Kituo cha Athi River Export Processing Zone, Kampuni ya  Coca Cola, mitaa ya  Mukuru, Imara Daima, North Airport road naEmbakasi. Maeneo mengine ni South B, Hospitali ya Mater, Makadara, Hamza na maeneo yote ya Mtaa wa  Industrial