×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 442 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona nchini

Watu 442 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona nchini

Kenya leo hii imerekodi asilimi 8.2 ya maambukizi ya korona baaada watu wengine mia nne arubaini na wawili kuthibitishwa kuambukizwa kufuatia kupimwa kwa sambuli elfu tano mia tatu ishirini na saba katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita na sasa kufikisha idadi jumla ya watu waliambukizwa kuwa elfu arubaini mia sita na ishirini.

Miongoni mwa waliombukizwa mia nne kumi na tisa ni Wakenya huku ishirini na watatu wakiwa raia wa kigeni. Aidha wa kiume ni mia mbili themanini na sita huku wa kike wakiwa mia moja hamsini na sita. Mtu mchanga zaidi ana umri wa miaka mitatu na mkubwa akiwa na umri wa miaka themanini na sita

Dakta Rashid Aman Katibu wa Utawala katika Wizara ametangaza takwimu za maambukizi ya korona akiwa katika Kaunti ya Uansi Ngishu.

Kwa mara kwanza Kaunti ya Nakuru imeorodeshwa kuongoza kwa maambukizi mapya huku ikirekodi watu tisini na wanne waliombukizwa ikifuata na Nairobi watu thamanini na kisha Mombasa arubaini na watatu.

Wazara ya Afya aimethibitisha kupona kwa watu mia moja sitini na sita huku mia moja arubaini wakiwa walioduhumiwa nyumbani na wangine ishirini na sita wakiwa waliokuwa wakihudumiwa hospitalini. Idadi hii sasa inafikisha watu elfu thelathini mia nane na sabini na sita.

Hata hivyo, watu wengine wanne wamefariki dunia kutokona na ugonjwa wa Covid-19 na sasa kufikisha mia saba hamsini na watano idadi jumla ya waliofariki dunia.