×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Odinga aandeleza shutma dhidi ya Ruto kutokana na misaada yake kwa vijana

Odinga aandeleza shutma dhidi ya Ruto kutokana na misaada yake kwa vijana

Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga ameendelea kumkabili Naibu wa Rais William Ruto kuhusu misaada yake anayoendelea kuitoa kwa Wakenya.

Akizungumza kwenye Kaunti ya Kisii, Raila amesema Ruto anatumia mbinu hiyo kuwafumba macho Wakenya kuhusu jinsi alivyokosa kuwasaidia kwa miaka yote minane ambayo amekuwa serikali kwa kuwapa Bero Wheelbarrow licha ya serikali ya jubilee kutoa ahadi chungu nzima wakati wa kampeni za mwaka 2013 vilevile mwaka 2017.

Raila ambaye amekutana kwa mara ya kwanza na hasimu wake Gavana wa Migori Okoth Obado kwenye kaunti hiyo, amewataka Wakenya kuwapuuza viongozi wanaopinga BBI, akisisitiza kwamba ndio suluhu pekee ya changamoto nyingi zinazolikumba taifa hili.

Wakati uo huo Seneta wa Siaya James Orengo amemtaka kuweka wazi tofauti zilizopo baina yake na Waziri wa Usalama wa Kitaifa Fred Matiang'i. Orengo amedai kwamba wakati wa kikao cha baraza la mawaziri jana, Ruto alishindwa kujibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na Rais Uhuru Kenyatta vilevile mawaziri kuhusu masuala ya usalama na jinsi wandani wake wanavyoendeleza siasa za mapema.

Kwa upande wao Gavana wa Kakamega na Granton Samboja wamewataka viongozi wa tangatanga kusitisha siasa za mapema na kutoa nafasi kwa serikali ya kitaifa vilevile za kaunti kuwahudumia Wakenya.