×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Baraza la Mawaziri limeidhinisha mwongozo kuhusu mikutano ya kisiasa

Baraza la Mawaziri limeidhinisha mwongozo kuhusu mikutano ya kisiasa

 Baraza la Mawaziri limeidhinisha maagizo ya Baraza la Kitaifa la Usalama kwamba mikutano yote ya kisiasa ni lazima iidhinishwe siku tatu kabla ya kufanyika. Baraza hilo  chini ya uwenyekiti wa Rais Uhuru Kenyatta aidha limeidhinisha uzinduzi wa kundi linalozishirikisha idara mbalimbali za serikali kudumisha nidhamu ya umma kufuatia kuanza kupanda kwa joto la kisiasa nchini.

Kamati hiyo itajumuisha wawakilishi wa Wizara ya Masuala ya Ndani ya nchi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Teknokojia na Mawasiliano, Idara ya Ujasusi, NIS, Tume ya Huduma za Polisi,  NPSC, Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano na Mamlaka ya Mawasilliano, CA.

Jukumu la kundi hilo ni kufuatilia, kunakili na kutekeleza maagizo mbalimbali kuhusu maandalizi ya mikutano ya umma na misafara ya kisiasa. Aidha litafuatilia mienendo ya watu mbalimbali yamatumizi ya mitandao ya kijamii vilevile taarifa zinazopeperushwa ili kuepusha vurugu nchini.

Hayo yakijiri, Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiang'i amesema hakuna mashinikizo yoyote ya kisiasa yatakayowafanya maafisa wa polisi kukosa kutekeleza majukumu yao yakiwamo ya kukabili ghasia wakati wa mikutano ya siasa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kidijitali wa Chama cha Ushirika cha Maafisa wa Polisi, Matiang'i amewataka wanasiasa kuwa makini kuhusu matamshi yao wanapohutubia umma kwani wanaweza kuligawanya taifa wasipokuwa makini.

Kauli ya Matiang'i imejiri huku baadhi ya wanasiasa hasa wanaomuunga mkono Naibu wa Rais, William Ruto wakiishtumu serikali kwa madai ya kuwatumia polisi kumkabili Ruto na wandani wake.