×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ruto alazimika kuahirisha mkutano wake katika Kaunti ya Nyamira

Ruto alazimika kuahirisha mkutano wake katika Kaunti ya Nyamira

Naibu wa Rais, William Ruto amelazimika kuahirisha mkutano wake katika Kaunti ya Nyamira baada ya polisi kuwatanya watu waliokuwa wamefika kuhudhuria mkutano wake. Badala yake, Ruto amesema mkutano huo utafanywa Alhamisi wiki ijayo huku akiwataka wakazi kusalia watulivu.

Kupitia mtandao wake wa Twitter, Ruto aidha amewashtumu polisi kwa kuvuruga mkutano wake ilhali hakuna aliyekuwa akipanga vurugu.

Ruto amechukua hatua hiyo baada ya mazungumzo na wabunge Vincent Kemosi wa Mugirango Magharibi,  Joash Nyamoko na Shadrack Mose wa Kitutu Masaba  vilevile Chama cha Ushirika cha Wahudumu wa Bodaboda.

 

Mapema leo, polisi wametumia vitoza-machozi kuwatawanya wakazi waliokuwa wakimsubiri katika Shule ya Upili ya Kebirigo, ambapo alitarajiwa kuongoza hafla ya kuchangisha fedha kwa wanabodaboda.

Ruto alitarajiwa kuhudhuria hafla hiyo saa nane leo hii baada ya mkutano wa Baraza la Mawaziri hapa jijini Nairobi.

Hata hivyo, Kemosi, Nyamoko na Mose wamekerwa na hatua ya polisi kuwatawanya watu waliofika.

Baadhi ya vijana na kina mama pia wameeleza kutoridhishwa na uamuzi huo kwani walikuwa wakimsubiri kwa hamu.