×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Polisi wamewatanya watu waliokuwa tayari kuhudhuria mkutano wa Ruto huko Nyamira

Polisi wamewatanya watu waliokuwa tayari kuhudhuria mkutano wa Ruto huko Nyamira

Maafisa wa polisi wamewatawanya watu waliokuwa wamekusanyika katika  uwanja wa Shule ya Msingi ya Kebirigo ambapo Naibu wa Rais William Ruto alitarajiwa kuongoza mmojawapo wa mikutano yake katika eneo la Nyamira.

Mamia ya watu  walikuwa wamekusanyika wakiwajumuisha wahudumuwa boda boda waliotarajiwa kuchangiwa, watumbuizaji na  waandalizi wa mikutano yake.

Hata hivyo mapema leo, taarifa kutoka kwa idara ya usalama Nyamira iliashiria kwamba mkutano huo hautaruhusiwa kutokana na masharti mapya ya kufanya mikutano ya hadhara.

Hata hivyo hatua hiyo imewakera baadhi ya waliotarajiwa kumpokea akiwamo Mbungewa Mugirango Magharibi Vincent Kemosi na wa Mugirango Kaskazini Joash Nyamoko.

Baadhi ya vijana na kina mama pia wameelezea kutoridhishwa na uamuzi huo kwani walikuwa wakimsubiri kwa hamu

Miongoni mwa masharti hayo ni kutolewa notisi ya mapema kwa wakuu wa polisi wa eneo ambapo mkutano unatarajiwa kufanyika lengo kuu likiwa kuzuia uhasama wa kisiasa nchini. Joseph Kinyua ni Mkuu wa Utumishi wa Umma.