×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watoto milioni 2 huzaliwa wakiwa wamefariki kila baada ya sekunde 16

Watoto milioni 2 huzaliwa wakiwa wamefariki kila baada ya sekunde 16

Watoto milioni mbili hufariki huzaliwa wakiwa tayari wamefariki dunia kila baada ya sekunde kumi na sita. Umesema Umoja wa Mataifa UN.

UN sasa inahofia kwamba janga la korona huenda likachangia zaidi ya watoto wengine elfu 200,000 kuzaliwa wakiwa tayari wamefariki dunia na kufanya hali kuwa mbaya zaidi duniani.

Ripoti ya umoja huo imesema kwamba asilimi 84 ya hali hiyo hutokea kwenye mataifa yenye viwnago vya chini vya ukuaji wa  uchumi kutokana na mifumo duni ya afya na ukosefu wa wakunga waliohitimu.

Shirikali linalowashughulikia  Watoto la umoja huo UNICEF, limesema kuwa suala la kuzaliwa kwa watoto wakiwa wamefariki linaweza kukabiliwa kupitia kuboreshwa kwa sekta ya afya na kuwapa akina mama mafunzo ya uzazi.

Ripoti hiyo ya pamoja ya UNICEF na Benki ya Dunia imesema kuwa hali hiyo huenda ikasababisha matatizo makubwa katika siku zijazo iwapo watoto wataendelea kuriki dunia kutokana na matatizo ambayo yangeweza kuepukika.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF, Henrietta Fore amesema janga la korona na hali duni ya sekta afya hasa Barani Afrika huenda likaongeza idadi ya watoto wanaozaliwa wakiwa wamefariki dunia.