×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Raila aahidi kumbwaga Ruto katika kinyang'anyiro cha Msambweni

Raila aahidi kumbwaga Ruto katika kinyang'anyiro cha Msambweni

Kinara wa ODM Raila Odinga amewataka wapinzani wa chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Eneo Bunge la Msambweni kujitayarisha kwa kinyanganyiro kikali. Raila hapo jana amemtambulisha rasmi mgombeaji wa chama cha ODM Omar Boga  kwa wapiga kura huku akitumia fursa kumsuta vikali Naibu wa Rais William Ruto ambaye vilevile anajiandaa kumpigia debe mgombeaji wa binafasi Feisal Abdalla Baddah.

Raila ameendeleza shutma zake kuhusu miradi ya Ruto kwa vijana kupitia ufadhili wa vifaa vya kazi kama vile bero, pikipiki mkokoteni na kadhalika akisema anfaa kufanya zaidi ili kuwawekea vijana hao mazinhira ya kunawiri.

Chama cha ODM  kimetaja uchaguzi huo mdogo kuwa nafasi nyingine ya kuwanyamazisha wale anaowataja kuwa maadui ya maendeleo na mabadiliko nchini na wasiowajali wakazi wa Msambweni.

Wagombejai wengine katika kinyangayiro hicho ni Bashir Kilalo wa KADU, Sharlet Akinyi ambaye ni mgombeaji huru na Dr Mohamed Mwakahonje wa chama cha United Green Movement.