×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mutyambai aagizwa kumrejeshea walinzi Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi

Mutyambai aagizwa kumrejeshea walinzi Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi

Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai, ameagizwa kumrejeshea walinzi Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi baada ya kuwapokonya walinzi wake.

Hakimu Mkuu Isaac Orenge amesema Sudi anastahili kupewa walinzi kwa mujibu wa sheria na kwamba ombi la Sudi kutaka walinzi wake warejeshwe halikusikilizwa.

Orenge amesema uamuzi wa Mutyambai kuagiza Sudi kupokonywa walinzi ilikuwa kunyume na sheria na unaolenga kumkandamiza mbunge huyo.

Hakimu huyo amesisitiza umuhimu wa kila Mkenya kusilikizwa na mahakama na malalamiko yake kushughulikiwa pasi na ubaguzi.

Sudi hapo jana aliwasilisha ombi kupinga hatua ya kupokonywa walinzi wake na kutaka warejeshwe mara moja.

Kupitia wakili wake Bernard Ng'etich, mbunge huyo alisema kuwa maisha yake yamo hatarini baada ya walinzi wake kuondolewa Septemba tarehe 14 alipojiwasilisha katika Kituo cha Polisi cha Langas mjini Eldoret akihusishwa na tuhuma za matamshi ya chuki.

Awali mahakama ilimzuiliwa kuendesha mikutano ya kisiasa hadi jana Oktoba tarehe sita.

Vikao vya kesi dhidi yake vitaendelea Oktoba 30.