×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Serikali kusambaza fedha kwenye shule mbalimbali kufikia kesho Alhamisiesho Alhamisi

Serikali kusambaza fedha kwenye shule mbalimbali kufikia kesho Alhamisiesho Alhamisi

Serikali itasambaza fedha kwenye shule za msingi na za upili za umma kufikia kesho Alhamisi ili kufanikisha mpango wa wanafunzi kurejea shuleni kwa awamu Jumatatu wiki ijayo.

Akizungumza mjini Kisumu wakati wa kuzikagua taasisi mbalimbali za elimu, Waziri wa Elimu Profesa Goerge Magoha aidha amesema serikali itawanunulia maski wanafunzi wanaotoka kwenye familia zisizojiweza ili kuwakinga na maambukizi ya virusi vya korona.

Magoha aidha ameutetea mpango wa wanafunzi wa Gredi ya nne, Darasa la Nane na Kidato cha Nnne akisema serikali inalenga kuutumia kutambua jinsi masomo yanavyoweza kurejelewa kwenye taasisi mbalimbali za elimu kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na Shirika la Afya Duniani WHO vilevile Wizara ya Afya nchini.

Hayo yanajiri saa chache baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu Knut Wilson Sossion kusisitiza kwamba ataendelea kutoa wito kwa serikali kuhakikisha kwamba inatoa fedha za matumizi kwa shule za umma kabla ya mwisho wa wiki hii.

Aidha Sossion amepuuzilia mbali madai kwamba serikali haijaweka mikakati kuwahakikishia usalama wanafunzi pamoja na walimu akisema hatua kubwa imepigwa.

Wizara ya Elimu ilisemaa shule hizo zitafunguliwa kwa muhula wa pili na masomo kuendelea kwa kipindi cha wiki kumi na moja kuanzia Oktoba 12 hadi Disemba 23.  Aidha zitafungwa kwa kipindi cha wiki moja pekee kuanzia Disemba 24 hadi Januari mosi mwaka 2021.