×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

KNUT yaendelea kuwahimiza wazazi kuhakikisha wanao wanarejea shuleni Jumatatu

KNUT yaendelea kuwahimiza wazazi kuhakikisha wanao wanarejea shuleni Jumatatu

Chama cha Kitaifa cha Walimu nchini KNUT kimeendeelea  kuwashauri wazazi kuhakikisha wanao wanarejea shuleni kuanzia wiki ijayo, ilivyoagiza Wizara ya Elimu.

Katibu Mkuu wa chama hicho Wilson Sossion, amesema kwamba hatua hiyo imeafikiwa kufuatia mashauriano na washikadau wote hivyo wanaopinga hawana sababu.

Sossion amesema kwamba wataendelea kutoa wito kwa serikali kuhakikisha kwmaba inatoa fedha za matumizi kwa shule za umma kabla ya mwisho wa wiki hii ili kuhakikisha kwamba masomo yanaendelea bila hitilafu.

Katibu Mkuu huyo amepuuzilia mbali madai kwamba serikali haijaweka mikakati kuwahakikishia usalama wanafunzi pamoja na walimu akisema hatua kubwa imepigwa.

Sossion ameyasema hayo baada ya Wizara ya Elimu kutangaza jana kwamba shule za msingi zitafunguliwa kuanzia juma lijalo kwa wanafunzi wa Gredi ya nne na darasa la nane, huku za upili zikifunguliwa kwa wale wa kidato cha nne.

Wizara hiyo ilisemaa shule hizo zitafunguliwa kwa muhula wa pili na masomo kuendelea kwa kipindi cha wiki kumi na moja kuanzia Oktoba 12 hadi Disemba 23.  Aidha zitafungwa kwa kipindi cha wiki moja pekee kuanzia Disemba 24 hadi Januari mosi mwaka 2021.