×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Oscar Sudi sasa anadai maisha yake yamo hatarini

Oscar Sudi sasa anadai maisha yake yamo hatarini

Mbunge wa Kapseret, Oscar Sudi sasa anadai maisha yake yamo hatarini.  Mbele ya Mahakama ya Nakuru, Sudi anataka Idara ya Polisi, NPS kushurutishwa kumrejeshea walinzi wake baada ya kupokonywa awali.

Kwa mujibu wa mawakili wake, Sudi ni mwanasiasa na anatangamana na umma kila uchao hivyo kuweka maisha yake hatarini bila walinzi.

Ombi hilo litasikilizwa kesho iwapo atarejeshewa walinzi au la. Mwezi uliopita, Sudi alifunguliwa mashtaka matatu; mawili ya uchochezi na moja la mienendo mibaya huku akiyapinga.

Hakimu wa Mahakama ya Nakuru, Lilian Arika alimzuia Sudi kuendesha mikutano yoyote ya kisiasa kati ya Septemba tarehe 23 na leo Oktoba tarehe 6 wakati ambapo vikao vya kesi hiyo vimeendelea. Sudi aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano pesa taslimu.