×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Shule kufunguliwa kuanzia tarehe 12 Oktoba

Shule kufunguliwa kuanzia tarehe 12 Oktoba

Wizara ya Elimu imetangaza kufunguliwa kwa shule kwa awamu kuanzia Oktoba 12 yaani Jumatatu ijayo huku watakaorejea siku hiyo wakiwa wanafunzi wa gredi ya 4, wale wa darasa la nane na kidato cha nne.

Katika taarifa, Wizara ya Elimu imesema kwamba shule hizo zitafunguliwa kwa muhula wa pili na masomo kuendelea kwa kipindi cha wiki kumi na moja kuanzia Oktoba 12 hadi Disemba 23.  Aidha shule hizo zitafungwa kwa kipindi cha wiki moja pekee kuanzia Disemba 24 hadi Januari mosi mwaka 2021.

Masomo ya muhula wa tatu yataanza Januari 4 hadi Machi kumi na tisa. Aidha kulingana na kalenda hiyo mpya ya masomo, Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane, KCPE utaanza Machi 22 na kukamilika Machi 24 huku ule wa Kitaifa wa Kidato cha Nne, KCSE ukifanyika kwa muda wa wiki tatu na siku mbili kuanzia  Machi 25 hadi Aprili 16.

Usahihishaji wa mitihani ya KCSE utafanyika baina ya Aprili 19 na Mei saba. Aidha tayari ada zote za mitihani kwa watahiniwa zipelipwa na serikali.

Wizara ya elimu imesema wakati wanafunzi hao wa gredi ya nne, darasa la nane na kidato cha nne  watakaporejea, kila shule ni lazima ihakikishe wanafunzi na watu wote watakaokuwa shuleni wanavalia maski ili kuzuia maambukizi ya virusi vya korona, kupimwa joto mwilini, kunawa mikono huku vieuzi vikitumiwa iwapo hakuna maji.

Wizara imekiri kwamba kutakuwa na changamoto ya kudumisha agizo la kutokaribiana japo hali hiyo haistahili kutumiwa kuwa kigezo cha kuwazuia wanafunzi kurejea shuleni. Shule zote zilitotumiwa kuwa maeneo ya karantini zimepuliziwa dawa za kuua viini kwa usimamizi wa Wizara ya Afya huku kila shule ikitengewa kituo cha afya ambacho kinaweza kutumiwa kwa huduma mbalimbali kipindi hiki cha korona. Wakuu wa shule wametakiwa kuhakikisha masharti yote yanazingatia.

Ikumbukwe vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za elimu zilifunguliwa kuanzia jana ili kutoa nafasi kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho wanaosomea kozi mbalimbali.

Share this: