×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sitajisalimisha kwa polisi, asema Nyoro

Sitajisalimisha kwa polisi, asema Nyoro

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro anasisitiza kwamba kamwe hatojiwasilisha kwa maafisa wa polisi.

Kiongozi huyo anadai kwamba ofisi ya Rai imekuwa ikitumika kuwakandamiza baadhi ya wanasiasa ambao wanamuunga mkono Naibu wa Rais William Ruto katika azma yake ya kuwania urais mwaka 2022. Aidha, amesema kwamba polisi wana mitambo maalum wanayoweza kutumia kubaini aliko na hivyo hana haja ya kujisalimisha kwani hajapokea mwaliko rasmi wa polisi.

Nyoro na mwenzake wa Kandara Alice Wahome jana walitakiwa kufika mbele ya Idara ya Upelelezi, DCi kufuatia ghasia zilizozuka eneo la Kenol, Kaunti ya Murang'a ambako watu wawili walifariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa.