×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Muda wa kupata matokeo ya Korona Kupunguzwa na Wizra ya Afya

Muda wa kupata matokeo ya Korona Kupunguzwa na Wizra ya Afya

Muda wa kupata matokeo ya vipimo vya  maambukizi ya virusi vya korona unatarajiwa kupunguzwa kutoka saa 24 hadi dakika 15 pekee iwapo vipimo vipya vilivyoidhinishwa na Shirika la Afya Duniani WHO vitaanza kutumika hapa nchini.

Akijibu maswali kupitia mtandao wa Twitter, Mkurugenzi wa Matibabu  katika Wizra ya Afya Dkt. Patrick Amoth amesema tayari WHO limenunua vifaa milioni 120 ambavyo vinatarajiwa kusambazwa kwa mataifa mbalimbali ili kuwezesha upimaji wa Korona.

Amoth amefafanua kwamba si vifo vyote ambavyo vimeripotiwa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita vilitokea katika kipindi hicho. Kwa mujibu wa Amoth, baadhi ya takwimu zimetokana na shughuli ya tathmini iliyoanzishwa na Wizara ya Afya ili kunakili visa ambavyo huenda vilisahaulika ama havikunakiliwa ili kuvijumuisha katika rekodi